Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 04:12

Jake Sullivan yupo Beijing kwa mazungumzo na Wang Yi wa China


Jake Sullivan (L) mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani akiwa na Wang Yi, waziri wa mambo ya nje wa China
Jake Sullivan (L) mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani akiwa na Wang Yi, waziri wa mambo ya nje wa China

Pande zote mbili zimesema mazungumzo hayo yalikuwa ya wazi, yenye nguvu na yenye kujenga

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Jake Sullivan na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi walikutana kwa siku ya pili mjini Beijing leo Jumatano, na kufanya mazungumzo yaliyogusia suala ikiwemo uwezekano wa mkutano kati ya wakuu wa nchi hizo mbili na mivutano katika South China Sea.

Pande zote mbili zimesema mazungumzo hayo yalikuwa ya wazi, yenye nguvu na yenye kujenga, huku shirika la habari la serikali la Xinhua likimnukuu Wang akisema kuwa ni muhimu kwa kuendeleza uhusiano wa China na Marekani, katika njia sahihi n ahilo liko kwa viongozi hao wawili.

Wawili hao walijadili mipango ya mazungumzo ya ngazi ya juu kwa viongozi katika wiki zijazo, kulingana na taarifa kutoka White House. Shirika la habari la Xinhua limesema kuwa wawili hao pia walijadili uwezekano wa kufanyika kwa mkutano kati ya Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa China Xi Jinping.

Forum

XS
SM
MD
LG