Hata hivyo mpaka sasa mawakili wanasema kuna dazeni za watu ambao bado wamezuiliwa katika uwanja wa ndege wa JFK huko jijini New York.
Jaji wa mahakama hiyo huko New York Jumamosi usiku ameamuru watu wenye viza halali waruhusiwe kuingia nchini.
Kadhlika Jaji huyo amebatilisha kwa muda amri ya kuwarudisha watu makwao ambao wamekwama katika viwanja vya ndege vya Marekani kufuatia amri ya kiutendaji iliyotangazwa na serikali ya Trump.
"Rufaa hizo zinauwezekano mkubwa wa kufanikiwa ikiwa itakubalika kuwa kuwaondosha watu hao na wengine wenye kadhia kama yao inavunja haki zao za kisheria na usawa wa kulindwa uliodhaminiwa na Katiba ya Marekani," Jaji Ann Donnelly ameandika katika uamuzi wake.