Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:18

Mapigano zaidi yazuka Ivory Coast.


Wafuasi wa upinzani ndani ya gari la Polisi huko Abidjan, Ivory Coast, Nov. 3, 2020, wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
Wafuasi wa upinzani ndani ya gari la Polisi huko Abidjan, Ivory Coast, Nov. 3, 2020, wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi.

Mapigano zaidi yalizuka juu ya kuchaguliwa tena kwa Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara Jumanne wakati mataifa ya Afrika Magharibi na Ufaransa yakitaka mazungumzo ya kumaliza mivutano juu ya kipindi chake cha tatu kilichopingwa.

Mivutano imefufua majeraha juu ya uchaguzi uliokuwa na mzozo mkubwa mnamo mwaka 2010 ambao ulileta vita vifupi vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, na kuua karibu watu 3,000.

Walau mtu mmoja aliuawa katika mji wa kati-mashariki wa M'Batto Jumanne wakati vurugu zilipoibuka kati ya jamii zinazopingana za kikabila juu ya muhula wa tatu wa Ouattara, wakazi wa eneo hilo walisema.

Watu wengine tisa walifariki dunia kutokana na ghasia katika miji mingine miwili Jumatatu wakati mahakama ya juu ya nchi hiyo ilithibitisha ushindi wa uchaguzi wa Ouattara.

XS
SM
MD
LG