Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:50

Israel yashambulia Ukanda wa Gaza wakati Netanyahu akikaribia kuhutubia bunge Marekani


Vikosi vya Israel vimefanya mashambulizi mapya Ukanda wa Gaza, Jumatano, saa chache kabla ya Waziri Mkuu wake, Benjamin Netanyahu kulihutubia Bunge la Marekani.

Mashambulizi hayo ya karibuni kabisa ya Israel yaliharibu nyumba katika miji ya mashariki ya Khan Younis kusini mwa Gaza na maelfu ya watu walilazimika kuelekea maeneo ya magharibi kutafuta makazi, wakaazi wamesema.

Huduma ya dharura ya kiraia ya Palestina imesema ilipokea simu za masikitiko kutoka kwa wakaazi waliokwama katika nyumba zao huko Bani Suhaila, mashariki mwa Khan Younis, lakini haikufanikiwaa kuufikia mji huo.

Madaktari baadaye walisema Wapalestina wawili waliuawa katika shambulizi la anga dhidi ya Bani Suhaila, ambapo tawi la wapiganaji wa Palestina, Hamas limesema kuwa wapiganaji walilipua bomu dhidi ya shehena ya wanajeshi wa Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG