Madaktari wa Gaza wamesema mashambulizi ya Israel yamewauwa Wapalestina 44, Gaza, Alhamisi, wakiwemo takriban 13 waliouwawa katika mashambulizi tofauti ya anga ya usiku kucha.
Madaktari wamesema shambulizi jingine la anga liliwauwa watu tisa karibu na kambi ya wakimbizi ya Pwani katika Jiji la Gaza, wakati shambulizi jingine liliuwa watu wanne katika mradi wa makazi karibu na Beit Lahiya kaskazini mwa Gaza.
Baadaye Alhamisi, mashambulizi ya anga yaliwauwa takriban Wapalestina 15 katika makazi mawili ya familia zilizohamishwa mashariki mwa Gaza, wakati shambulizi tofauti la Israeli liliuwa takriban watu watatu katika kitongoji cha Jiji la Gaza.
Katika baadhi ya mashambulizi, Israel imesema inalenga vituo vya kamandi ya Hamas, bila kutoa ushahidi.
Forum