Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:10

Israel yaimarisha ulinzi katika ukanda wa magharibi


Wanajeshi wa Israel wakiwa katika oparesheni kwenye sehemu ya Jenin, ukingo wa magharibi April 12 2022. PICHA: AFP
Wanajeshi wa Israel wakiwa katika oparesheni kwenye sehemu ya Jenin, ukingo wa magharibi April 12 2022. PICHA: AFP

Wanajeshi wa Israel wameimarisha ulinzi katika ukanda wa magharibi, baada ya washambuliaji wa kipalestina kuua watu 14, raia wa Israel katika mashambulizi manne tofauti, katika wiki za hivi karibuni.

Jeshi la Israel limerithibitisha kutekeleza mashambulizi kadhaa katika ukanda wa magharibi na kuwakamata washukiwa 20.

Shughuli za jeshi la Israel zimeendelea katika mji wa Jenin, kaskazini mwa ukanda wa magharibi, ambako washambuliaji wawili wa kipalestina waliwaua waisarel.

Jumanne, Polisi wamesema kwamba Polisi wa Isreal alimpiga risasi na kumuua mwanamme mpalestina, aliyemchoma kisu kusini mwa Israel.

Matukio hayo ni sehemu ya visa vinavyotokea Isreal wakati huu wa mwezi wa Ramadan, huku o hali ya wasiwasi kati ya Isreal na Palestina imeongezeka sana.

mwezi wa Ramadan mwaka huu unaadimishwa sambamba na maadhimisho ya siku muhimu kwenye kalenda ya wayahudi na wakristo.

XS
SM
MD
LG