Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 01:08

Israel yafanya shambulizi mjini Beirut na kumlenga kamanda wa Hezbollah


Jengo lililoharibiwa na shambulizi la anga la Israel katika vitongoji vya kusini mwa Beirut, Julai 30, 2024. Picha ya AP.
Jengo lililoharibiwa na shambulizi la anga la Israel katika vitongoji vya kusini mwa Beirut, Julai 30, 2024. Picha ya AP.

Jeshi la Israel Jumanne jioni lilisema lilifanya shambulizi mjini Beirut likimlenga kamanda wa Hezbollah ambaye linadai alihusika na shambulio la anga ambalo liliua watoto 12 na vijana waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wa mpira mwishoni mwa juma katika milima ya Golan.

Mlipuko mkubwa ulisikika, na moshi mwingi ulionekana ukitanda juu ya vitongoji vya kusini mwa Beirut, ngome ya wanamgambo wa Hezbollah wanaofadhiliwa na Iran.

Afisa wa Hezbollah alisema majengo kadhaa yaliharibiwa na mamlaka ilisema watu wawili waliuawa.

Ripoti za vyombo vya habari huko Mashariki ya Kati zilimtambulisha kamanda wa Hezbollah kama Fuad Shukr, lakini hatma yake ilikuwa haijajulikana.

Chombo cha habari cha Saudia Al Hadath kiliripoti kwamba Shukr alinusurika. Lakini tovuti ya habari ya Israel Ynet ilinuku chanzo cha usalama cha Israel kikisema, “kuna uwezekano mkubwa afisa huyo wa Hezbollah aliuawa. Ikiwa alikuwa katika jengo hilo, hayuko nasi tena.”

Forum

XS
SM
MD
LG