Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:48

Israel yaelezea upatikanaji wa maiti za mateka


Maafisa wa Israel, Alhamisi wametoa maelezo ya jinsi walivyopata miili ya mateka watano waliouwawa wakati wa shambulizi la Oktoba la Hamas dhidi ya Israel, huku jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi yake huko Gaza.

Katika mkutano na wanahabari mjini Tel Aviv, msemaji wa jeshi Daniel Hagari amesema miili ya mateka hao imeshikiliwa na Hamas kwenye mahandaki ya mita 20 chini ya mitaa ya mji wa kusini wa Khan Younis.

Amesema miili hiyo ilipatikana Jumatano chini ya eneo ambalo hapo awali lilitengwa kama eneo la masuala ya kibinadamu na jeshi la Israeli.

“Eneo la raia wa Gaza kuhama kutoka uwanja wa vita na kupokea misaada ya kibinadamu na makazi,” Hagari amesema.

Hamas ilitumia vibaya eneo la juhudi za kibinadamu na kulitumia kuwashikilia mateka.

Forum

XS
SM
MD
LG