Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:54

Israel yadondosha makombora kwenye mji wa Rafah


Nyumba za makazi zilizoharibiwa na makombora ya Israel mjini Rafah Jumatatu. Feb 12,2024.
Nyumba za makazi zilizoharibiwa na makombora ya Israel mjini Rafah Jumatatu. Feb 12,2024.

Mashambulizi ya yanga ya Israel Jumatatu yamedondosha makombora kwenye mji wa Rafah na kuuwa takriban watu 70, kulingana na maafisa wa afya wa Ukanda wa Gaza, ambapo tayari kuna takriban wakazi milioni 1.4 waliotoroka kutoka maeneo mengine ya Gaza ili kuepuka mapigano.

Wakazi wanasema wameshuhudia makombora yakidondoka karibu na kambi ya wakimbizi, makazi ya watu pamoja na misikiti. Jeshi la Israel kwa upande wake limesema kwamba lililenga ngome za magaidi ndani ya Rafah, na kwamba wakati wa operesheni hiyo wamefanikiwa kuokoa mateka wawili wa Israel wenye asili ya Argentina, waliokuwa wanashikiliwa na wanamgambo wa Hamas.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepongeza operesheni hiyo, akisema kwamba taifa lake halitapoteza nafasi hata moja ya kurejesha mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza. “ Shinikizo la kijeshi hadi ushindi, ndilo pekee litakalopelekea kuachiliwa kwa mateka wote,” amesema Netanyahu.

Zaidi ya miezi 4 ya mapigano pamoja na amri za kuondoka kwa wakazi kutoka Gaza zimewasababisha wapalestina wa kanda hiyo yote kuhamia upande wa kusini, wengi wao wakiishi kwenye makambi ya Umoja wa Mataifa, yenye misongamano mikubwa karibu na mji wa Rafah.

Forum

XS
SM
MD
LG