Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:16

Maelfu wakimbia makazi yao Gaza


Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia nyumba zao katika mji wa Gaza Jumapili baada ya Israel kuwaonya waondoke kabla ya mfululizo mwingine wa mashambulizi katika siku ya sita ya mashambulizi ambayo maafisa wa Palestina wanasema yameuawa watu wasiopungua 160.

"Wale ambao hawatafuata maelekezo watahatarisha maisha yao na maisha ya familia zao," vikaratasi vilivyoangushwa na jeshi la Israel katika mji wa Beit Lahiya vilisema.

Licha ya kuongezeka kwa hatua za kijeshi za Israel - ikiwa ni pamoja na shambulizi la makomando wakati wa usiku katika kile Israel ilichosema ni operesheni ya ardhini - wapiganaji wa Hamas wameendelea kurusha roketi kuvuka mpaka.

Makomando walishambulia kile Israel ilichosema ni eneo la kurushia roketi. Maafisa wanasema wanajeshi wanne wa Israel walijeruhiwa katika mapigano ya bunduki na wapiganaji wa kipalestina.

XS
SM
MD
LG