Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:58

Israel na Uturuki kurejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia


Uturuki na Israel, Jumatano zimesema zitateua mabalozi wa kuziwakilisha ikiwa ni zaidi ya miaka minne baada ya kuwarejesha mabalozi wao nyumbani.

Hatua hiyo inaelezwa kuonyesha njia njema katika miezi kadhaa ya kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.

Mataifa hayo muhimu katika ukanda wao yaliwafukuza mabalozi wao 2018 baada ya kuuwawa Wapelestina 60 na vikosi vya Israel wakati wa maandamano ya ukanda Gaza kupinga kufunguliwa kwa ubalozi wa Marekani wa Jerusalem.

Lakini mataifa hayo yamekuwa yakijishughulisha kurejesha uhusiano wa muda mrefu ambapo sasa suala la nishati linaonekana kama eneo muhimu linaloweza kuleta ushirikiano.

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Yair Lapid, Jumatano imesema mataifa hayo mawili yamekubaliana kurejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia.

XS
SM
MD
LG