Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 01, 2024 Local time: 10:29

Israel imepiga kambi za kijeshi za Iran


Picha inayoonyesha muonekano wa Tehran baada ya kushambuliwa na Israel Octoba 26, 2024
Picha inayoonyesha muonekano wa Tehran baada ya kushambuliwa na Israel Octoba 26, 2024

Israel imesema kwamba imekamilisha shambulizi kubwa dhidi ya Iran baada ya zaidi ya mwaka mzima wa mapigano yaliyoanza kwa wanamgambo wa Hamas wanaofadhiliwa na Iran kuishambulia Israel.

Mapigano hayo yamepelekea vita vingine vinavyoihusisha Tehran moja kwa moja na washirika wake katika mashariki ya kati.

Katika taarifa ya mapema leo jumamosi, jeshi la ulinzi la Israel limesema kwamba ndege za kivita za Israel zimerudi salama baada ya kutekeleza mashambulizi ya uhakika dhidi ya kambi za kijeshi katika sehemu tofauti nchini Iran.

Taarifa imetolewa karibu saa nne baada ya kutolewa ripoti za kwanza za milipuko nchini Iran, saa nane na nusu usiku kwa saa za Tehran.

Msemaji wa jeshi la Israel Rear Admiral Daniel Hagari ameambia waandishi wa habari kwamba malengo ya mashambulizi ya angani ya Israel yamefanikiwa.

Shirika la habari la serikali ya Iran IRNA limenukuu idhra ya ulinzi ya Iran ikisema kwamba mashambulizi ya Israel yamelenga kambi za kijeshi mjini Tehran, na katika mikoa ya Khuzestan na Ilam, na kwamba makombora kadhaa yamenaswa, na kuongezea kwamba uharibifu ulikuwa mdogo.

Forum

XS
SM
MD
LG