Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 21:26

ISIS waongeza mashambulizi Syria


Mpiganaji wakiwa na bendera ya ISIS nchini Syria
Mpiganaji wakiwa na bendera ya ISIS nchini Syria

Ripoti kutoka Syria zinasema kwamba wapiganaji wanaohusishwa na Islamic State wameongeza mashambulizi mashariki na kati mwa taifa hilo katika siku za karibuni. 

Shirika la habari la North Press limesema kwamba takriban wanajeshi wawili wa serikali wameuwawa Jumatatu wakati wa shambulizi kutoka kwa watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa ISIS, karibu na mji wa kale wa Palmyra katikati mwa Syria.

Ripoti zinasema kwamba wapiganaji walilenga kituo cha uchaguzi cha jeshi la Syria wakati wakitumia gari la kijeshi lililokuwa limeibwa. Vyombo vya habari vya kieneo vimesema kwamba kabla ya tukio hilo, wanajeshi wengine 7 wa serikali ya Syria pamoja na wapiganaji wanao ungwa mkono na Iran waliuwawa mashiriki mwa Syria.

Kundi la ISIS limeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya wapinzani wao nchini Syria na Iraq licha ya kupoteza karibu kila sehemu lililoshikilia. Russia na Iran ndio waungaji mkono wakubwa wa serikali ya Syria ya rais Bashar al Assad.

Kulingana na kundi linalofuatilia hali katika eneo hilo la Syrian Observatory, ndege za Russia Jumatatu zilifanya takriban mashambulizi 15 ya anga kwenye maficho yanayoaminika kuwa ya wanamgambo.

XS
SM
MD
LG