Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 01, 2024 Local time: 02:50

Iraq na eneo la Kikurdi yadaiwa kukataa wakimbizi wa Syria


Mamlaka za Iraq, mjini Baghdad na utawala katika eneo lenye mamlaka kiasi  la Kikurdi, kaskazini mwa Iraqi wamekuwa wakiwazuia kiholela na kuwafukuza wakimbizi wa Syria nchini mwao, kundi kubwa la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema Alhamisi.

Shirika la Human Rights Watch lenye makao yake makuu jijini New York, limesema kuwa limeandikisha kesi ambapo serekali ya Iraq iliwafukuza Wasyria ingawa walikuwa na ukaazi halali au walikuwa wamesajiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

Wasyria waliripoti kukamatwa katika uvamizi wa maeneo yao ya kazi au mitaani, huku nyakati nyingine katika ofisi za makazi wakati wakijaribu kuandikisha vibali vyao.

Kwa mujibu wa UNHCR, Iraq inawahifadhi wakimbizi wa Syria wasiopungua 260,000, huku takriban asilimia 90 wakiishi katika eneo linalojitawala la Wakurdi kaskazini mwa Iraq.

Forum

XS
SM
MD
LG