Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 10:08

Iran yakaidi matakwa ya kimataifa ya kudhibiti mpango wake wa nyuklia


Bendera ya taasisi ya nguvu ya atomiki ya kimataifa (IAEA) wakati wa mkutano huko Vienna, Austria, Feb. 6, 2023. (AP)
Bendera ya taasisi ya nguvu ya atomiki ya kimataifa (IAEA) wakati wa mkutano huko Vienna, Austria, Feb. 6, 2023. (AP)

Iran imekaidi matakwa ya kimataifa ya kudhibiti mpango wake wa nyuklia na imeongeza hifadhi yake ya uranium iliyorutubishwa hadi kufikia viwango vya kuwa  silaha, kulingana na ripoti ya siri ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuangalia nyuklia

Iran imekaidi matakwa ya kimataifa ya kudhibiti mpango wake wa nyuklia na imeongeza hifadhi yake ya uranium iliyorutubishwa hadi kufikia viwango vya kuwa silaha, kulingana na ripoti ya siri ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuangalia nyuklia iliyoonekana siku ya Jumanne na The Associated Press.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ilisema hadi Oktoba 26, Iran ina kilo 182.3 za urani iliyorutubishwa hadi asilimia 60, ongezeko la kilo 17.6 tangu ripoti ya mwisho ya Agosti.

Uranium iliyorutubishwa kwa usafi wa asilimia 60 ni hatua fupi tu ya kiufundi mbali na viwango vya silaha vya asilimia 90.

Forum

XS
SM
MD
LG