Imran Khan, Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, amewasilsiha maombi rasmi ya kugombea nafasi ya kansela wa chuo kikuu cha Oxford kutoka jela, msaidizi wake wa karibu ametangaza Jumapili.
Khan alihudumu kama kiongozi wa Pakistan kuanzia mwaka 2018 hadi Aprili 2022 wakati alipoondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye iliyoitishwa na katika bunge ambayo alidai ilipangwa na jeshi lililo na nguvu la Pakistan.
“Kulingana na maelekezo ya Imran Khan, fomu yake ya maombi kwa Chuo Kikuu cha Oxford 2024 imewasilishwa,” Sayed Zulfiqar Bukhari alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter. “Tunatarajia uungaji mkono wa kila mtu kwa kampeni ya kihistoria,” aliandika.
Forum