Mahakama ilimlinda Khan dhidi ya kukamatwa hadi Septemba mosi kwa tuhuma kwamba wakati wa hotuba mwishoni mwa juma, aliwatishia maafisa wa polisi na hakimu mwanamke. Matukio hayo kabla ya ahueni ya mahakama kwa Khan yalizua hofu ya makabiliano makali kati ya polisi na Khan, ambaye anaongoza mikutano ya hadhara na kutaka uchaguzi wa haraka baada ya kuondolewa madarakani.
Serikali inasema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa mwaka ujao.
Siku ya Alhamisi, Khan aliwaambia wanahabari nje ya mahakama kwamba hakuwahi kutishia mtu yeyote.
Alisema mashtaka ya ugaidi dhidi yake yamechochewa kisiasa na kwamba serikali ya Waziri Mkuu Shahbaz Sharif inahofia umaarufu wa Khan unaoongezeka.