Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:07

IEBC yatoa hesabu kamili ya wapiga kura kwa mahakama


kikao cha mahakama kinachosikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Dr. William Ruto kama rais mteule, kenya
kikao cha mahakama kinachosikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Dr. William Ruto kama rais mteule, kenya

Tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC imetetea namna ilivyoandaa uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na kusema kwamba ulifanyika kwa njia huru na haki, ikisisitiza kwamba inajua vizuri zana idadi ya wapiga kura waliojitokeza.

Wakili wa IEBC Mahat Somane, ameiambia mahakama ya juu inayosikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Dr. William Ruto kama rais mteule, kwamba idadi ya wapiga kura iliyotangazwa na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati, Agosti 15 ni sawa na haikupunguzwa wala kuongezwa.

Raila Odinga amepinga ushindi wa Ruto akisema kwamba ulikumbwa na dosari kubwa na wizi wa kura na kwamba haijulikani idadi kamili ya wapiga kura walioshiriki zoezi hilo.

IEBC imeiambia mahakama kwamba wapiga kura 14,326,751 walishiriki zoezi hilo, ikiwa ni asilimia 64.77 ya wapiga kura 22,120,458 waliosajiliwa kupiga kura kote Kenya, katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Idadi ya wapiga kura waliotambuliwa na KIMS pamoja na daftari la kawaida

Wakili Somane amesema kwamba idadi ya wapiga kura milioni 14.33 walitambuliwa kwa njia ya teknolojia ya kisasa (KIEMS) na kwa daftari la kawaida la karatasi.

Wapiga kura 14,239,862 walitambuliwa kwa kutumia KIEMS katika vituo vya kupigia kura 45,994 kati ya vituo 46,229.

Wapiga kura 86,889 walitambuliwa kwa kutumia daftari la kawaida la karatasi katika vituo 229.

Kaunti za Makueni na Kakamega ni baadhi ya sehemu ambazo vifaa vya KIMS vilikosa kufanya kazi siku ya uchaguzi.

Odinga amedai kwamba idadi ya kura za urais zilizojumulishwa hailingani na idadi ya wapiga kura waliojitokeza.

Kulingana na Odinga, idadi ya wapiga kura waliojitokeza Agosti 9, ni zaidi ya asilimia 65.4

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati alimtangaza Dr. William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kura milioni 7.18 (Asilimia 50.49) ikilinganishwa na kura milioni 6.94 (Asilimia 48.85) za Raila Odinga.

Makamishna 4 wapinga idadi ya wapiga kura iliyotangazwa na IEBC

Makamishan wanne wa IEBC Juliana Cherera, Justus Nyang’aya, Irene Masit na Francis Wanderi waliongea na waandishi wa habari Agosti 16 muda mfupi kabla ya matokeo rasmi kutangazwa na kusema kwamba kulikuwa na kura 142,000 zaidi ya idadi ya wapiga kura walioshiriki zoezi hilo.

Walidai kwamba matokeo yaliyotangazwa na Chebukati yalizidi kwa asilimia 0.001.

Kulingana na makamishna hao, asilimia 0.01 ilikuwa sawa na kura 142,000.

“Asilimia ya jumla ya kura za urais inafikia 100.01 ambayo ni kura 142,000 zaidi ya idadi ya wapiga kura waliojitokeza”, alisema Cherera.

Cherera alidai kwamba pamoja na makamishna wenzake watatu, walimwambia mwenyekiti wa tume hiyo kuhusu idadi ya kura lakini alikataa kuwasikiliza.

XS
SM
MD
LG