Idara ya usalama ya Sudan imepiga marufuku kusafiri kwa wanachama wa kikosi kazi kinachosimamia mabadiliko ya nchi hiyo kuelekea demokrasia, vyanzo vya serikali vilisema, wakati mivutano kati ya viongozi wa kiraia na wanajeshi ikitishia kuongezeka zaidi wiki kadhaa baada ya mapinduzi yaliyofeli.
Mgogoro huo wa kisiasa ulizuka Septemba 21, wakati Waziri Mkuu Abdalla Hamdok aliposema wanajeshi hatari ambao bado watiifu kwa kiongozi wa zamani Omar al-Bashir walipotaka kwa nguvu kuvuruga mapinduzi ambayo yalimwondoa rais huyo wa zamani mamlakani mwaka 2019.
Vyanzo viwili vya juu vya serikali ya raia vilisema Jumatano kwamba marufuku hayo ya kusafiri ya Idara ya Ujasusi (GIS) iliathiri maafisa 11 wa kiraia wengi wao wakiwa wajumbe wa Kamati waliopewa jukumu la kumaliza urithi wa kifedha na kisiasa wa Bashir.
Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa GIS au wawakilishi wa jeshi.
Vyanzo vilisema orodha hiyo ni pamoja na Mohamed al-Faki, ambaye katika mkutano na waandishi wa habari mwezi uliopita alilaumu wanajeshi kwa kutumia mapinduzi kama kisingizio cha kujaribu kutwaa madaraka.