Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:11

Idara ya ujasusi ya Somalia yakamata silaha zinazodaiwa kwenda kwa Al Shabab


Idara ya kitaifa ya ujasusi ya Somalia (NISA) Alhamisi imesema kuwa imekamata shehena mbili haramu za silaha na vifaa vya milipuko ambavyo vinaonekana kuwa vinaelekea kwa kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Waziri wa ulinzi wa Somalia, Mohamed Ali Haga, idara hiyo ilipata silaha hizo kwenye bandari na uwanja wa ndege wa Mogadishu.

“Kwenye bandari ya Mogadishu, wafanyakazi wa NISA waligundua shehena ya silaha na vifaa vya vilipuzi vilivyofichwa ndani ya makontena kama bidhaa za biashara zilizoidhinishwa kutoka nje ya nchi,” Haga alisema.

Ameendelea kusema kwamba maafisa wetu walikamata zana za kijeshi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden Ade mjini Mogadishu. Taarifa kutoka NISA imesema uchunguzi kuhusiana na shehena hizo haramu ulisababisha kukamatwa kwa watu 10 wanaohusishwa na mtandao wa magendo.

XS
SM
MD
LG