Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:19

Idadi ya watu nchini Tanzania imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 37 hadi milioni 61.7


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia taifa. March 19, 2021.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia taifa. March 19, 2021.

Idadi ya watu nchini Tanzania iliongezeka kwa zaidi ya asilimia 37 katika muongo mmoja hadi milioni 61.7, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Jumatatu, akionya changamoto zinazoletwa na ongezeko la idadi hiyo ya watu alipokuwa akizindua matokeo ya sensa ya kitaifa.

Mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania Dar es Salaam unakaribia kuwa mojawapo ya majiji yenye watu wengi zaidi duniani katika miaka ijayo.

Idadi ya watu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki iliongezeka kutoka milioni 44.9 mwaka 2012 hadi zaidi ya milioni 60, kulingana na sensa iliyofanyika mapema mwaka huu, huku Hassan akisema idadi hiyo ilionyesha ongezeko la kila mwaka la asilimia 3.2.

Idadi ya watu kama hii inaweza isiwe jambo kubwa kwa nchi kubwa kama yetu lakini ni mzigo linapokuja suala la kutenga rasilimali na kutoa huduma za kijamii," Hassan alisema wakati wa hafla iliyotangazwa moja kwa moja kutoka mji mkuu Dodoma.

Tunahitaji mikakati ya maendeleo kuwahudumia watu hawa," alisema.

Dar es Salaam imesalia kuwa mkoa wenye wakazi wengi zaidi wenye takriban wakazi milioni 5.4, wakati visiwa vya Zanzibar vina watu wapatao milioni 1.9, ikiwa ni ongezeko la watu 600,000.

XS
SM
MD
LG