Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:48

Idadi ya vifo kutokana na dawa za kulevya Marekani yashuka


Picha ya dawa za kulevya aina ya cocaine zilizokamatwa Ujerumani miaka kadhaa iliopita. Julai 2019.
Picha ya dawa za kulevya aina ya cocaine zilizokamatwa Ujerumani miaka kadhaa iliopita. Julai 2019.

Kushuka kwa vifo kutokana na utumizi kupita kiasi wa dawa za kulevya hapa Marekani  mwaka huu kumetoa matumaini kwa wataalam kwamba hatua muhimu zimepigwa katika kupambana na janga hilo.

Ndani ya miezi 12 iliopita hadi Juni 30 mwaka huu, kulikuwa na vifo 97,000 kutokana na dawa za kulevya kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatano kutoka Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa. Idadi hiyo imeshuka kwa asilimia 14 kutoka vifo 113,000 vilivyoripotiwa mwaka uliotangulia.

Barndon Marshal ambaye ni mtafiti kutoka chuo kikuu cha Brown amesema kuwa inaridhisha kuona idadi ya vifo kutokana na dawa za kulevya ikiwa imeshuka kwa haraka. Vifo kutokana na utumizi kupita kiasi wa dawa za kulevya vilianza kuongezeka kwenye miaka ya 90, zaidi kutokana na dawa za kuzuia maumivu za opioid na herion, na katika miaka ya karibuni dawa za fentanyl.

Takwimu zanaonyesha kuwa idadi ya vifo ilianza kushuka mwaka jana, na ripoti ya Jumatano inaonyesha kwamba hali hiyo inaendelea. Ripoti hiyo imeongeza kuwa utumizi wa dawa za kulevya umeshuka kwenye majimbo 45 ya Marekani, wakati ukiongezeka Alaska, Nevada, Oregon, Utah na Washington.

Forum

XS
SM
MD
LG