Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:16

Watu wapatao 200 wafariki Japan


Magari na takataka nyingine zikiwa katika kifusi kilichobebwa na mawimbi ya tsunami kaskazini mwa Japan.
Magari na takataka nyingine zikiwa katika kifusi kilichobebwa na mawimbi ya tsunami kaskazini mwa Japan.

Mitetemeko kadha midogo inaendelea kutokea sehemu mbali mbali. Huduma nyingi za umma ikiwa ni pamoja na usafiri zimesimamishwa

Taarifia mpya zinasema idadi ya watu waliokufa Japan mpaka sasa inafikia 200 na itaongezeka kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililopiga mwambao wa kaskazini-mashariki ya Japan na kusababisha mawimbi ya tsunami yenye urefu wa hadi mita 10. Mawimbi hayo yamezoa maboti, nyumba na magari katika mwambo ya bahari ya Pacific. Idadi ya vifo imetangazwa kufikia 40 lakini maafisa wanaamini itaongezeka sana.

Picha za video kutoka maeneo ya pwani iliyokumbwa na tsunami zinaonyesha eneo kubwa likipigwa na mawimbi yaliyoyojaa na matope na takataka za kila aina katika eneo la mashamba la Sendal.

Uharibifu mkubwa unaonekana dhahiri katika miji kadha ya mwambao. Katika eneo la Chiba mtambo mkubwa wa kusafishia mafuta ulipasuka na kusababisha moto.

Mjini Tokyo, mamia ya kilomita kutoka kitovu cha tetemeko, majengo yalitikisika kwa nguvu na bidhaa kuanguka kutoka katika makabati. Paa la jumba moja kubwa lilianguka. Tetemeko hilo kali limepiga majira ya usiku wa mapema Ijumaa.

XS
SM
MD
LG