Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:12

ICC yataka kukamatwa kwa viongozi wa Russia


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu – ICC, imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Shoigu na Mkuu wa Majeshi ya Russia, Jenerali Valery Gerasimov.

ICC Jumanne imesema kuna ushahidi wa kuridhisha na kuaminika kuwa washukiwa hao wawili wanawajibika kwa mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi la Russia, dhidi ya miundombinu ya umeme ya Ukraine kati ya Oktoba 2022 na Machi 2023.

Mahakama imeitolea mfano wa mashambulizi ya Russia, ambayo yalilenga mitambo na vituo vidogo vya Ukraine.

Taarifa ya ICC imesema Shoigu na Gerasimov wanadaiwa kuhusika na kuelekeza mashambulizi kwenye maeneo ya raia na kusababisha madhara makubwa kwa raia, ambayo yote ni uhalifu wa kivita.

Forum

XS
SM
MD
LG