Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 01:22

ICC inasema inafuatilia kwa makini hali ya kisiasa nchini Venezuela


Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu- ICC, Karim Khan
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu- ICC, Karim Khan

Maduro kiongozi wa muda mrefu Venezuela alitangazwa mshindi wa uchaguzi dhidi ya mpinzani wake González

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC Karim Khan amesema Jumatatu kwamba ofisi yake ipo makini inafuatilia hali huko Venezuela kufuatia uchaguzi wake wa urais uliokuwa na mzozo.

Nicolás Maduro, kiongozi wa muda mrefu wa kisoshalisti nchini Venezuela, alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Julai 28 dhidi ya mpinzani wake Edmundo González, na kumpatia Maduro muhula wa tatu. Viongozi wa upinzani wanadai Gonzalez alipokonywa ushindi.

Tangu uchaguzi, wafuasi wa maduro wamewakamata Zaidi ya watu 2,000 ambao waliandamana au kuhoji ushindi wake, licha ya ushahidi unaoeleza kwamba alishindwa uchaguzi kwa pointi mbili kwa moja. Maandamano tangu upigaji kura yamesababisha vifo vya watu 24.

Forum

XS
SM
MD
LG