Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:57

Upinzani Afrika Kusini wapinga serikali kutaka kujiondoa ICC


Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Michael Musutha alipotangaza nchi kujiondoa uanachama wa ICC.
Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Michael Musutha alipotangaza nchi kujiondoa uanachama wa ICC.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Democratic Alliance (DA) kinapanga kuwasilisha changamoto kwenye mahakama ya katiba Jumatatu kupinga uamuzi wa serikali kujiondoa katika uanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) yenye makao yake The Hague.

Hatua hii imekuja baada ya Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Michael Musutha kusema kuwa serikali itawasilishwa mswaada bungeni kwa wabunge kufuta saini ya nchi hiyo kwenye mkataba wa Roma ambao umeunda ICC.

Ijumaa, Afrika Kusini iliijulisha rasmi Umoja wa Mataifa kwamba inataka kujiondoa kutoka ICC.

Lakini mbunge James Selfe, mmoja wa wanachama katika kundi la masuala ya sheria kwenye DA amesema serikali ya Rais Jacob Zuma imekosea kikatiba kuieleza Umoja wa Mataifa kabla ya kupaa ridhaa ya bunge la Afrika Kusini.

“Democratic Alliance imechukizwa na uamuzi huu. Tunadhani inapeleka ujumbe ambao si sahihi kabisa kuhusu nia yetu ya dhati kwa haki za binadamu na kuchukizwa kwetu na ukiukaji wa haki za binadamu na mauaji ya halaiki, na tunaamini kwamba itaturudisha nyuma katika sera yetu ya mambo ya nje na jinsi ambavyo Afrika Kusini itakavyoonekana kwa njia ambazo ni za msingi kabisa,” amesema Selfe.

Uamuzi wa Afrika Kusini kuanza utaratibu wa kujiondoa ICC unakuja siku kadhaa baada ya bunge la Burundi kuidhinisha pendekezo la serikali ya Bujumbura kutaka kujiondoa kwenye mahakama hiyo ya The Hague.

XS
SM
MD
LG