Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 18:55

Hungary kuchukua uongozi wa muda wa EU, Jumatatu


Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban, akiwasili mjini Brussels. Juni 27, 2024
Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban, akiwasili mjini Brussels. Juni 27, 2024

Hungary  Jumatatu inachukua uongozi wa  kupokezana wa Umoja wa Ulaya, wakati ikiahidi kuongoza kwa uadilifu, licha ya wasi wasi mwingi kutokana na kile wakosoaji wanachokiona kuwa utawala wa kiimla, na urafiki wao mkubwa na serikali ya  Russia.

Waziri Mkuu wa taifa hilo Viktor Orban, ambaye ameliongoza taifa hilo la Ulaya ya kati tangu 2010, wakati akijitahidi kulifanya kuwa la demokrasia ya kilibelari, licha ya mzozo wa mara kwa mara na Brussels, kuhusu utawala wa kisheria na haki za binadamu.

Orban ndiye kiongozi pekee wa Ulaya aliyedumisha uhusiano na Russia, licha ya uvamizi wa Ukraine. Kufikia sasa amekataa kutuma silaha kwa Kyiv, huku akikosoa vikwazo ilivyowekewa Russia kutokana na vita hivyo. Mwaka jana bunge la Ulaya lilitoa pendekezo likiangazia kuzembea kwa Hungary kwa thamini za demokrasia, wakati likihoji uwezo wake wa kuongoza EU kwa muda wa miezi 6.

Hata hivyo Budapest imesisitiza iko tayari kuongoza Umoja huo wenye mataifa 27 wanachama. ”Tutakuwa wapatanishi wenye haki, kwa ushirikiano wa wanachama wote, pamoja na taasisi,” amesema waziri wa Hungary kwenye maswala ya EU, Janos Boka.

Forum

XS
SM
MD
LG