Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:12

Human Rights Watch yadai Rwanda imeuwa wakosoaji wake waliopo nje ya nchi


Tirana Hassan, mkurugenzi mkuu wa Human Rights Watch akiwa Geneva, Uswizi, Machi 30, 2023.
Tirana Hassan, mkurugenzi mkuu wa Human Rights Watch akiwa Geneva, Uswizi, Machi 30, 2023.

Shirika la Human Rights Watch le Jumanne limesema kwamba  serikali ya Rwanda imeua, kushambulia pamoja na kuwapoteza wakosoaji wake waliopo nje ya nchi, suala ambalo linahitaji kukemewa na jumuia ya kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taifa hilo ndogo la Afrika Mashariki limetawaliwa na rais Paul Kagame tangu mauaji ya kimbari ya 1994, wakati akipanga kuwania tena wadhifa huo kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao. HRW lenye makao yake makuu Marekani limetoa ripoti hiyo baada ya kufanya mahojiano na watu 150, likiangazia miaka tangu ushindi wa Kagame kwenye uchaguzi wa 2017.

Ripoti hiyo imeorodhesha zaidi ya kesi darzeni moja za mauaji, utekaji nyara, majiribio ya utekaji nyara na mashambulizi dhidi ya raia wa Rwanda wanaoishi kwenye mataifa ya kigeni, wakati kukiwa na majarbio ya kuwarejesha nyumbani. Shirika la habari la AFP lilipowasiliana na msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo kuhusu suala hilo amesema kwamba HRW imeendelea kutoa taarifa potofu ambazo ziko katika mawazo yao tu.

Forum

XS
SM
MD
LG