Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:31

HRW yatoa wito kufanyika uchunguzi huru Eswatini


Waandamanaji waliokuwa wakidai mageuzi ya kidemokrasia Eswatini
Waandamanaji waliokuwa wakidai mageuzi ya kidemokrasia Eswatini

Wito huo umekuja wakati Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa alitarajiwa kuzuru Eswatini hii leo Jumanne kwa mazungumzo na mfalme Mswati wa tatu kuhusu maendeleo ya kisiasa na kiusalama katika ufalme huo, Pretoria ilisema

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) Jumanne lilitoa wito wa uchunguzi huru kufuatia ukamataji wa waandamanaji ambao uliibuka Eswatini, ufalme wa mwisho kabisa barani Afrika hapo mwezi June.

Wito huo umekuja wakati Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa alitarajiwa kuzuru Eswatini hii leo Jumanne kwa mazungumzo na mfalme Mswati wa tatu, kuhusu maendeleo ya kisiasa na kiusalama katika ufalme huo, Pretoria ilisema.

Ramaphosa mwezi uliopita alituma wapatanishi baada ya kuzuka kwa maandamano mapya huko Eswatini. Mamia ya watu wamejeruhiwa tangu maandamano yalipozuka kwa mara ya kwanza mwezi Juni katika machafuko mabaya zaidi kuwahi kulikumba koloni la zamani la uingereza ambalo kwa kawaida lilikuwa na amani.

Mfalme Mswati wa tatu wa Eswatini
Mfalme Mswati wa tatu wa Eswatini

Watu 46 waliuawa mwezi Juni huku wengine wasiopungua 245 wakijeruhiwa kwa risasi kulingana na HRW ikinukuu ripoti za hivi majuzi za kundi linalofuatilia haki katika eneo. Waathiriwa walionusurika walisema walipigwa risasi na wanajeshi iliongeza HRW.

XS
SM
MD
LG