Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:31

Honduras imefungua ubalozi wake mjini Beijing huko China


Waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang (L) na mwenzake wa Honduras, Enrique Reina wakizindua ishara ya kufunguliwa ubalozi huko Beijing. June 11, 2023. Xinhua News Agency
Waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang (L) na mwenzake wa Honduras, Enrique Reina wakizindua ishara ya kufunguliwa ubalozi huko Beijing. June 11, 2023. Xinhua News Agency

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang na mwenzake wa Hondura, Enrique Reina walishiriki katika uzinduzi wa ubalozi huo siku ya Jumapili, kituo rasmi cha CCTV ya China kimesema. Ripoti hiyo imesema Honduras bado inahitaji kuamua eneo la kudumu la ubalozi huo na itaongeza idadi ya wafanyakazi wake

Honduras ilifungua ubalozi wake mjini Beijing siku ya Jumapili vyombo vya habari vya serikali ya China vimeripoti miezi kadhaa baada ya taifa hilo la Amerika ya Kati kuvunja uhusiano na Taiwan ili kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang na mwenzake wa Hondura, Enrique Reina walishiriki katika uzinduzi wa ubalozi huo Jumapili asubuhi, kituo rasmi cha CCTV ya China kimesema. Ripoti hiyo imesema Honduras bado inahitaji kuamua eneo la kudumu la ubalozi huo na itaongeza idadi ya wafanyakazi wake.

Hata hivyo waziri Qin aliahidi kuwa China itaanzisha mfumo mpya na Honduras wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo zenye ukubwa na mifumo tofauti kulingana na taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya China.

Ishara ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa pande hizo mbili imekuja wakati wa ziara ya siku sita, ya Rais wa Honduras, Xiomara Castro nchini China.

Forum

XS
SM
MD
LG