“Tunawaomba wajumbe wa Baraza la Usalama kutumia nguvu zao za pamoja ili kusaidia kulinda watu waliojikuta katika mapigano hayo,” Martha Pobee, msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika, aliwaambia wajumbe wa baraza hilo.
Duru nyingine ya mapigano makubwa yalizuka Septemba 12 kati ya vikosi vya akiba, ambavyo vilisonga mbele kwenye mji mkuu wa El Fasher kutoka pande nyingine dhidi ya vikosi vya jeshi la Sudan, ambavyo viko ndani ya mji huo.
El Fasher ndio mji mkuu pekee katika eneo la Darfur ambao bado haujaangukia kwa wanamgambo wanaofanya uasi.
Forum