Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 09:57

Guterres azitaka Russia na Ukraine kusitisha harakati za kijeshi karibu na kiwanda cha nyuklia cha Ukraine


Kiwanda cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia. Picha ya Reuters
Kiwanda cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia. Picha ya Reuters

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres Alhamisi ametoa wito wa kusitisha harakati za kijeshi karibu na jengo la kiwanda cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia, huku Moscow na Kyiv zikilaumiana kwa mashambulizi mapya ya makombora.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilikutana jana kujadili hali hiyo.

Russia ilikiteka kiwanda hicho kikubwa cha nyuklia barani Ulaya mwezi Machi baada ya kuivamia Ukraine tarehe 24 Februari.

Kiwanda hicho bado kinaendeshwa na mafundi wa Ukraine.

Kampuni ya nishati ya Ukraine Energoaton imesema eneo hilo lilishambuliwa mara tano jana Alhamisi, ikiwemo karibu na kituo kunakofifadhiwa vifaa vya mionzi.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema katika taarifa kwamba makombora ya Ukraine yameharibu kwa kiasi mtambo wa kuzalisha umeme wa joto na madimbwi ya maji ambayo ni sehemu ya mifumo ya baridi.

Guterres amehimiza kuondolewa kwa wanajeshi na zana za kijeshi na kusipelekwe wanajeshi na zana zaidi.

Ametoa wito kwa Russia na Ukraine kutolenga viwanda na eneo linalozunguka viwanda hivyo.

“Kiwanda hicho hakipaswi kutumiwa kama sehemu ya operesheni yoyote ya kijeshi. Badala yake, makubaliano ya haraka yanahitajika kwenye ngazi ya kiufundi katika eneo salama lisilokuwa na harakati za kijeshi ili kuhakikisha usalama wa eneo,’’ Guterres amesema katika taarifa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishtumu Russia kutumia kiwanda hicho cha nyuklia “kutishia dunia nzima.”

XS
SM
MD
LG