Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 01:10

Guinea yawasilisha rasimu ya katiba mpya inayopunguza muda wa muhula wa urais


Serikali ya mpito ya Guinea imewasilisha rasimu ya katiba mpya ambayo itapunguza na kuweka ukomo wa mihula ya urais, na uwezekano wa kumruhusu kiongozi wa sasa wa kijeshi Mamady Doumbouya kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais.

Serekali ya kijeshi iliyochukua madaraka kwa mapinduzi ya 2021 ilipendekeza kipindi cha mpito cha miaka miwili kuelekea uchaguzi mwaka 2022 baada ya kufanya mazungumzo na jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi, lakini imeonyesha dalili ndogo za kutekeleza hayo.

Rasimu ya katiba mpya, inayotarajiwa kupigiwa kura ya maoni ambayo bado haijaamuliwa, inaweza kufungua njia kwa taifa hilo la Afrika Magharibi linalozalisha madini ya bauxite na chuma kurejea katika utawala wa kikatiba.

Nakala mpya, iliyowasilishwa Jumatatu katika Baraza la Kitaifa la Mpito, ambalo linafanya kazi kama bunge chini ya serikali ya mpito, haikukataza maafisa wa serikali ya kijeshi kushiriki mchakato wa uchaguzi.

Rais wa zamani Alpha Conde, 86, aliye-pinduliwa na wanajeshi karibu miaka mitatu iliyopita, hatajumuishwa kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na ukomo wa umri.

Iwapo rasimu ya katiba mpya itaidhinishwa, rais atachaguliwa kwa muhula wa miaka mitano unaoweza kuongezwa mara moja, na hivyo kupunguza muhula wa urais kutoka miaka sita katika katiba iliyoidhinishwa mwaka wa 2020. Bado haijafahamika mpaka sasa ni lini uchaguzi wa rais utafanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG