Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 10:00

Global Fund yasuta ripoti za rushwa


Dk. Michel Kazatchkine mkurugenzi wa Global Fund kutoka Ufaransa akizungumza na waandishi habari Lausanne, Uswisi.
Dk. Michel Kazatchkine mkurugenzi wa Global Fund kutoka Ufaransa akizungumza na waandishi habari Lausanne, Uswisi.

Maafisa wa tasisi ya kimataifa ya kupambana na ukimwi kifua kikuu na malaria, wanakosoa ripoti za hivi karibuni katika vyombo vya habari juu ya matumizi mbaya wa msaada wa tasisi hiyo ya Global Fund.

Maafisa hao wanasema ripoti hizo zinatokana na matukio yaliyotokea na kuchukuliwa hatua mwaka jana na hakuna habari mpya.

Kwa hakika matumizi mbaya ya misaada ya Global Fund si tatizo jipya, limetokea katika baadhi ya nchi za Afrika na inaonekana hatua huchukuliwa. Lakini kile Global Fund lalamika ni ripoti za vyombo vya habari zinazodai kwamba ulaji rushwa unachukua sehemu kubwa kutoka misaada ya mabilioni ya dola inayotolewa na Global Fund kwa wakati huu. Na zinadai kwamba hadi theluthi mbili katika baadhi za misada hutumiwa kwa njia ya wizi.

Mkurugenzi mtendaji wa tasisi hiyo Michel Kazatchkine anasema Global Funda ina sera ya kutosthamilia kamwe rushwa na hutafuta kwa dhati kufichua ushahidi wowote wa utumiaji mbaya wa fedha.

Anasema matukio yanayotajwa katika ripoti za hivi karibuni kwenye vyombo vya habari yanahusu utumiaji mbaya sana wa fedha katika nchi 4 kati ya 145 zinazopokea msaada. Amesema kesi hizo zilichukua nafasi ya juu kabisa katika ripoti ya mwaka jana ya mkaguzi mkuu wa serikali.

Kazatchkine anasema, “Matokeo yake ni kwamba, hatua za haraka zilizchukuliwa huko Djibuti, Mali, Mauriutania na Zambia, kutafuta fedha zilizotumiwa vibaya na kuzuia utumiaji mbaya wa fedha za msaada katika siku za mbele. Kwa ujumla Global Fund inadai kukusanya dola milioni 34 ambazo hazijulikani zilizpo katika nchi hizo na nchi nyenginezo, kati ya jumla ya dola bilioni 13 zilziotolewa.”

Kazatchkine anasema, kesi za uhalifu zinaendelea huko Mali, Mauritania na Zambia. Anasema tasisi imesitisha misaada muhimu kwa Mali na Zambia.

Anasema uwazi ni nguzo ya msingi katika kazi zote za tasisi yake. Anaongeza kusema Global Fund inawajibikja kwa wafadhili wake kuhusiana na matumizi yake, na inadhamira ya kuzuia utumiaji mbaya wa fedha zake.

Mkurugenzi wa Global Fund anasema, “kinacho nitia wasi wasi mimi, bila shaka, ni kwamba jambo hili linasababisha mtikiso mkubwa kupita maoni jumla ya raia kwa namna fulani wakati huu ambao serikali za dunia zinakabiliwa na kishinikizo cha kupunguza matumizi ya umaa na ambapo mamilioni ya watu wanaoitegemea Global Fund na matumaini Global Fund inaleta duniani huwenda yakawa hatarini.”

Kazatchkine anasema, maisha ya watu elfu nne wanaougua na Ukimwi, kifua kikuu na malaria yanaokolewa kila siku kutokana na fedha za msaada zinazotolewa na tasisi hiyo.

Anasema tasisi hiyo na afisi ya mkaguzi mkuu zinazidisha juhudi kuzuia ubadhirifu. Alisema zile zinazojulikana kama nchi zenye hatari zinafuatiliwa kwa karibu zaidi ili kuhakikisha hakuna fedha zinazotoweka.

XS
SM
MD
LG