Polisi nchini Misri wamekuwa wakizozana na waandamanji walojawa na hamaki kudhibiti uwanja wa Tahriri Square kutokana na kuendelea kwa jukumu la majeshi katika siasa za Misri. Maafisa wa kutoa huduma za afya wanasema watu 3 waliuwawa Jumapili na mamia ya wengine kujeruhiwa. Maandamano hayo sasa yanasambaa nje ya mji mkuu. Waandamanji walimiminika barabarani katika miji ya Cairo, Alexandria, Suez na kwingineko Jumapili wakipambana na vikosi vya ulinzi katika ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu maandamano ya mwamko hapo mwezi Januari. Maandamano hayo yamefanyika wiki tu kabla uchaguzi wa bunge kufanyika.
Polisi watumia virungu na mabomu ya machozi kwa maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali ya kijeshi kuendelea kukaa madarakani Misri.