Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 19:00

Ghasia mpya zanukia Tigray


Kifaru kilichoharibiwa kwenye mapigano ya awali ya Tigray
Kifaru kilichoharibiwa kwenye mapigano ya awali ya Tigray

Mzozo ulioko kaskazini mwa Ethiopia katika eneo la Tigray, Jumatano umeonyesha dalili za kuongezeka baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed, kuashiria kumalizika kwa tangazo la kusitisha mapigano.

Tangazo hilo limekuja wakati eneo jirani la Amhara likisema kuwa litaendelea na mashambulizi dhidi ya vikosi vya Tigray. Vikosi vya Tigray People’s Liberation Front, TPLF, ambavyo tayari vilikuwa vimeshika tena udhibiti wa maeneo mengi katika kipindi cha wiki 3 zilizopita baada ya sitisho la mapigano, vimeapa kuchukua tena eneo hilo lenye rutuba upande wa magharibi na lililochukuliwa na vikosi vya Amhara wakati wa mapigano ya awali.

Waziri mkuu Abiy Ahmed mwezi uliopita aliondoa vikosi vya serikali kuu kutoka kwenye maeneo mengi ya Tigray ikiwa kama hatua ya kusitisha mapigano, hatua iliotajwa na TPLF kuwa mzaha, kwa kuwa wanajeshi wake walishindwa.

Tangazo la Jumatano linaonekana kubadili msimamo, baada ya kiongozi huyo kusema kuwa sitisho la mapigano halijasaidia. Msemaji wa serikali ya kieneo ya Amhara amesema kuwa wanatayarisha vikosi vyao ili kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Tigray.

Shirika la habari la reuters linasema kuwa msemaji huyo hata hivyo hajafafanua zaidi kuhusu hatua ya kundi lake ambalo pia linajulikana kama FANO.

Magharibi mwa Tigary kwa muda mrefu imekuwa nyumbani kwa watu kutoka makabila ya Tigrinya na Amhara na sasa ghasia mpya kati ya makundi hayo mawili, huenda zikapelekea wimbi jipya la wakimbizi. Tayari wakimbizi milioni mbili wametoroka makwao tangu ghasia zilipozuka Novemba mwaka uliopita.

XS
SM
MD
LG