Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:00

Ghana imekimbilia IMF kwa mkopo, hali ya uchumi ni mbaya


Rais wa Ghana Nana Akufo
Rais wa Ghana Nana Akufo

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amehutubia taifa na kuahidi kwamba serikali yake inachukua hatua maalum kutatua mgogoro wa uchumi unaokumba taifa hilo.

Addo amesema kwamba hatua zinazochukuliwa ni za haraka pamoja na za mda mrefu, kuhakikisha kwamba Ghana inapata ukuaji wa uchumi.

"Tupo katika mgogoro, sifanyi mzaha ninaposema hivyo. Siwezi kupata mfano katika historia wakati changamoto nyingi zinapokuja pamoja kwa wakati mmoja. Lakini tutashughulikia mgogoro huo namna tumeshughulikia changamoto ambazo tumekumbana nazo katika siku zilizopita, sio tu kupata suluhisho la mda mfupi na la dharura, bali pia la mda mrefu."

Ghana inafanya mazungumzo na shirika la fedha duniani IMF, kupata msaada wa kifedha kukabiliana na changamoto zake za kiuchumi inazokumbana nazo kwa sasa.

"Tumeomba msaada wa shirika la fedha duniani IMF kutusaidia kukarabati uchumi wetu kwa sasa, wakati tunafanya kazi kuweka mikakati ya mda mrefu ya kujenga uchumi ulio dhabithi na kujenga Ghana isiyotegemea misaada."

Bei ya chakula na bidhaa muhimu imepanda kwa kiwango kikubwa nchini Ghana huku sarafu yake ukishuka thamani.

Katika hotuba yake ya nusu saa, rais Nana Akufo-Addo, ametangaza mikakati kadhaa ya kujenga uchumi wa nchi hiyo, ikiwemo kuimarisha uzalishaji wa bidhaa.

XS
SM
MD
LG