Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:12

Ghailani kuhukumiwa Jan. 25


Mwendesha mashitaka wa Marekani akitoa maelezo katika kesi ya Ahmed Khalfan Ghailani, mjini New York Oktoba 2010.
Mwendesha mashitaka wa Marekani akitoa maelezo katika kesi ya Ahmed Khalfan Ghailani, mjini New York Oktoba 2010.

Waendesha mashitaka wa serikali kuu Marekani wamemtaka jaji wa mahakama moja ya New York kumpa hukumu ya kifungo cha maisha Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani atakapopewa hukumu Januari 25 baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika ulipuaji mabomu wa ubalozi wa Marekani mjini Dar es salaam mwaka 1998.

Novemba 17, 2010 Ghailani mwenye umri wa miaka 36 alikutwa hana hatia katika mashitaka 280 ya kula njama na mauaji katika shambulizi hilo, lakini alikutwa na hatia katika shitaka moja la kula njama kuharibu mali ya serikali ya Marekani. Anakabiliwa na hukumu ya lazima ya miaka 20 gerezani.

Serikali ya Marekani hapo Januari 11 ilipinga dai la upande wa utetezi kutaka Mtanzania huyo afanyiwe kesi upya. Upande wa utetezi unadai kuwa hatia ya Ghailani inafaa kufutwa ama kesi ifanywe upya.

Lakini serikali ya Marekani inashikilia kuwa ushahidi unaonyesha kuwa Ghailani "alinunua gari lililojazwa milipuko uliyotumika kushambulia ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

XS
SM
MD
LG