Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:30

George Clooney azungumzia tatizo la Sudan


George Clooney na babake wakiandamana Washington mbele ya ubalozi wa Sudan
George Clooney na babake wakiandamana Washington mbele ya ubalozi wa Sudan

Clooney alisema wameshuhudia mamia ya watu wakikimbilia kwenye milima kujificha wakihofia usalama wao na hilo linatokea kila siku.

Mcheza filamu mashuhuri na mtetezi wa haki za binadamu wa Marekani George Cooney amewaonya wabunge wa marekani Jumatano kuhusu mzozo wa kibinadamu katika mpaka wa Sudan na Sudan Kusini ambapo wakazi wanakimbilia maeneo ya milima ya Nuba kutokana na ulipuaji mabomu unaofanywa kiholela. Clooney alisema wameshuhudia mamia ya watu wakikimbilia kwenye milima kujificha wakihofia usalama wao na hilo linatokea kila siku. Clooney alielezea kamati ya masuala ya kigeni ya seneti ya Marekani jinsi alivyosafiri kwa siri kuvuka mpaka kwenda kwenye milima ya Nuba nchini Sudan ambako alikabiliwa na shambulizi la roketi na kushuhudia vifo na madhara mengine. Aliongeza kuwa watu katika eneo hilo wanahofia maisha yao kutokana na njaa au mashambulizi ya risasi na mabomu.

XS
SM
MD
LG