Rais aliyepo madarakani Ivory Coast anasema atachukua udhibiti wa matawi ya benki ya Afrika magharibi katika juhudi za kudhibiti tena fedha za serikali na kushikilia madaraka.
Bw. Gbagbo amewataka wafanyakazi wa Ivory Coast kujibu kwa maafisa wa nchi hiyo na sio utawala wa benki ambao makao yake yako Dakar Senegal Bw. Gbagbo anahitaji kupata uwezo kwa mali za serikali ili aweze kulipa wafuasi wake katika serikali na jeshi.
Katika hatua ya kujibu, mshindi anayetambulika kimataifa wa uchaguzi wa Novemba Allasane Ouattara ametoa amri kwa matawi ya benki hiyo huko Ivory Coast kufungwa . Na ameahidi kumshitaki mtu yeyote atakayefuata amri ya Bw. Gbagbo.