Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:27

Gavana wa benki kuu Libya asema amelazimika kuondoka nchini pamoja na wafanyakazi wengine wa benki


Gavana wa Benki Kuu ya Libya, Siddiq al-Kabir wakati wa mahojiano na Reuters mjini Tripoli, Libya Septemba 1, 2021.
Gavana wa Benki Kuu ya Libya, Siddiq al-Kabir wakati wa mahojiano na Reuters mjini Tripoli, Libya Septemba 1, 2021.

Gavana wa benki kuu ya Libya Sadiq al-Kabir alisema yeye na wafanyakazi wengine wakuu wa benki wamelazimika kuondoka nchini humo ili  kulinda maisha yao kutokana na mashambulizi yanayoweza kufanywa na wanamgambo wenye silaha, gazeti la Financial Times liliripoti Ijumaa.

Wanamgambo wanawatishia na kuwatia hofu wafanyakazi wa benki na wakati mwingine wanawateka nyara watoto wao na jamaa zao ili kuwalazimisha kwenda kazini, Kabir aliliambia gazeti hilo kwa njia ya simu.

Pia alisema majaribio ya Waziri Mkuu wa muda Abdulhamid al-Dbeibah kumuondoa kwenye nafasi yake yalikuwa kinyume cha sheria, na yalikiuka makubaliano ya mashauriano ya Umoja wa Mataifa juu ya udhibiti wa benki kuu.

Mgogoro wa udhibiti wa Benki Kuu ya Libya unasababisha kiwango kingine cha ukosefu wa utulivu katika nchi ambayo ni mzalishaji mkuu wa mafuta, taifa ambalo limegawanyika kati ya upande wa mashariki na magharibi ambazo zinapata uungwaji mkono kutoka Uturuki na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG