Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:54

Gavana wa zamani wa New Mexico Bill Richardson afariki dunia


Hayati Gavana Bill Richardson wakati wa uhai wake katika Umoja wa Mataifa akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi Machi 26, 1998. AP.
Hayati Gavana Bill Richardson wakati wa uhai wake katika Umoja wa Mataifa akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi Machi 26, 1998. AP.

Bill Richardson, gavana wa mihula miwili mdemokrat wa New Mexico aliyewahi kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ambaye alijitolea maisha yake baada ya kustaafu siasa kufanya kazi kutafuta suluhu ya Wamarekani waliokamatwa nje ya nchi amefariki dunia .

Kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2002 kama Gavana, Richardson alikuwa balozi wa Umoja wa Mataifa na waziri wa nishati chini ya Rais Bill Clinton na alihudumu kwa miaka 14 kama mbunge anayewakilisha New Mexico

Alikuwa na umri wa miaka 75. Kituo cha Richardson for Global Engagement, alichoanzisha na kukiongoza kilisema katika taarifa yake Jumamosi kwamba alifariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake Chatham, Massachusetts.

Richardson pia alisafiri kote ulimwenguni kama msuluhishi asiye rasmi wa kidiplomasia, akitafuta suluhu ya kuachiliwa kwa mateka na wanajeshi wa Marekani kuanzia Korea Kaskazini, Iraqi, Cuba hadi Sudan.

Forum

XS
SM
MD
LG