Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:49

Gambia kujiondoa kwenye ICC


Rais wa Gambia Yahya Jammeh.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh.

Gambia Jumanne imeshutumu mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC, kwamba haitilii maanani uhalifu wa kivita, kabla ya kuashiria kujiondoa kwa uanachama wa mkataba uliounda mahakama hiyo.

Gambia Jumanne imeshutumu mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC, kwamba haitilii maanani uhalifu wa kivita, kabla ya kuashiria kujiondoa kwa uanachama wa mkataba uliounda mahakama hiyo wa Roma. Gambia sasa inajiunga na Burundi na Afrika Kusini, nchi ambazo pia zimeshiria kujiondoa kwenye mahakama hiyo mapema mwezi huu.

Waziri wa habari wa Gambia, Sheriff Bojang aliushutumu mfumo unaotumiwa na mahakama hiyo kwa kile alichokiita kuwa ubaguzi na kwamba mahakama hiyo imekuwa ikiwalenga waafrika pekee.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, waziri huyo alisema kuwa Gambia ilichukua hatua hiyo kwa sababu,licha ya ICC kuitwa ya kimataifa, mahakama hiyo ni ya wazungu na inatumiwa tu kuwashtaki watu wengine ambao si wazungu, hasa waafrika.

Kesi tisa kati ya kumi zinazochunguzwa na mahakama hiyo ya ICC zimelenga nchi za kiafrika, jambo ambalo limewafanya baadhi ya wagambia kuamini kuwa haina nia ya kuwafungulia mashtaka raia kutoka mataifa mengine.

XS
SM
MD
LG