Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 26, 2025 Local time: 20:40

Fulgence Kayishema, mtoro wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda kuomba hifadhi nchini Afrika Kusini


Fulgence Kayishema (kushoto) akizungumza na wakili wake Juan Smuts (kulia) katika Mahakama ya Cape Town, tarehe 26 Mei 2023. Picha na RODGER BOSCH / AFP.
Fulgence Kayishema (kushoto) akizungumza na wakili wake Juan Smuts (kulia) katika Mahakama ya Cape Town, tarehe 26 Mei 2023. Picha na RODGER BOSCH / AFP.

Fulgence Kayishema,mmoja wa watoro wa mwisho waliokuwa wanatafutwa kwa kuhusika kwao katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, ataomba hifadhi nchini Afrika Kusini, ambako amekuwa akiishi kwa miongo miwili, wakili wake alisema Jumanne.

“Maagizo yangu ni kuomba hifadhi katika Jamhuri ya Afrika Kusini,” wakili Juan Smuts aliiambia AFP baada ya Kayishema kufika mahakamani mjini Cape Town.

Smuts amesema mteja wake anahofia usalama wake, ikiwa atarejeshwa nchini mwake.

Kayishema ambaye alikuwa anatafutwa na wachungunzi wa Umoja wa mataifa, alikamatwa mwezi uliopita katika mji wa Paarl katika mkoa wa Afrika Kusini wa Cape Winelands.

Inadaiwa alishiriki katika moja ya matukio ya umwagaji damu mkubwa wa mauaji ya halaiki, wakati maelfu ya wanaume, wanawake na watoto ambao walikuwa wametafuta hifadhi katika kanisa waliuawa kikatili.

Forum

XS
SM
MD
LG