Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 10:38

Papa Francis awaasa wapinga mabadiliko


Papa Francis yuko kwenye ziwa takatifu la Namugongo. Novemba 2015.
Papa Francis yuko kwenye ziwa takatifu la Namugongo. Novemba 2015.

Papa Francis awaeleza maaskofu na makadinali wa kanisa katoliki kuwa Vaticn ni lazima ijibadilishe ili kukabiliana na na mahitaji ya leo ya kanisa.

Papa Francis Alhamisi amewalaumu wanaopinga mabadiliko katika uongozi wa Vatican, akisema baadhi ya upinzani huo ni shinikizo la shetani na wale mapadri ambao wanafanya kazi naye lazima waendelee kujitakasa ili kulitumikia kanisa katoliki vizuri zaidi.

Kwa mwaka wa tatu mfululizo wa malumbano, Francis ameupa changamoto uongozi wa Vatican katika salamu zake za krismas.

Ameongeza kusema mchakato wa mabadiliko, ambao ilikuwa sababu ya kuchaguliwa kwake.

Aliongeza kuwa nia yake siyo kuleta mabadiliko bandia kwa uongozi wa Holy See, lakini ni mabidiliko thabiti katika fikra za wale wanaoshirikiana nae katika uongozi.

“Ndugu zangu, siyo matatizo katika kanisa ambayo mnatakiwa muyaogope, lakini ni yale madoa ya kudumu!”

Mwaka 2014, Francis alishtushwa na uongozi wa Vatican pale alipo orodhesha “maradhi ya kiroho” 15 ambayo yanawakabili viongozi wake. Aliwashutumu kutumia nafasi zao kunyang’anya madaraka na mali, kuishi maisha ya “kinafiki” katika sura mbili na kujisahau- lililotokana na “maradhi ya usahaulifu wa kiroho” – kwamba wanatakiwa kuwa na mapenzi ya kuncha mungu.

Mwaka jana, Francis “aliorodhesha mema” ambayo wanatakiwa kutenda, yakiwemo uaminifu, kujizuilia na maovu, heshima na unyenyekevu.

Mwaka huu aliwapa viongozi wadini wakiwemo maaskofu na makadinali wanaofanya kazi chini yake miongozo 12 inayohamasisha mchakato wa mabadiliko, iliyo husisha kuunganisha idara mbalimbali za Vatican na kuunda nyingine mpya.

Alisema Vatican lazima ijibadilishe ili kuweza kukabiliana na mahitaji ya kanisa la leo, Francis amesema alitaka Vatikan iwe ni ya mseto na ihusishe waumini wa kawaida wakikatoliki, hasa wanawake, katika kufanya maamuzi. Pia anasisitiza juu ya wafanyakazi wake kuwa na taaluma ya juu.

Kwa kiwango kikubwa, ametoa wito “kusitishwa kabisa” utaratibu uliopo Vatican wa kuwaondosha wafanyakazi wasio na ujuzi au wenye matatizo, ambao unajulikana kama “pandisha cheo na fukuza kazi.”

“Hii ni saratani!” Francis amesema.

XS
SM
MD
LG