Maafisa kutoka Uturuki, Finland na Sweden, Ijumaa wamekubaliana kuendelea kukutana katika miezi kadhaa ijayo kujadili hali ya usalama.
Hali wasiwasi huo ulianzishwa na Uturuki ikiwa ni masharti ya awali ili kuruhusu mataifa hayo mawili ya Nordic kujiunga na ushirika wa NATO.
Maafisa kutoka mataifa matatu wamefanya mkutano kama huo Ijuma katika mji wa Finland wa Vantaa.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufini, Pekka Haavisto, amesema mkutano huo unalenga kuanzisha mawasiliano na kuweka malengo ya ushirikiano ambayo mataifa hayo yalikubali kusaini masharti ya NATO katika mkutano wa Madrid wa mwezi Juni.
Mataifa hayo mawili yaliomba kujiunga na NATO ikiwa ni mwitikio baada ya Russia kuivamia Ukraine, lakini yalikabiliwa na upinzani kutoka Uturuki ambayo inazishutumu nchi hizo kwa kuweka vikwazo dhidi ya Ankara na kuunga mkono wale inaowachukulia kuwa ni magaidi.