Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:41

Filamu ya 'The Death of Stalin' matatani Russia


Wapita njia wakiangalia tangazo la filamu ya 'The Death of Stalin' nchini Urusi
Wapita njia wakiangalia tangazo la filamu ya 'The Death of Stalin' nchini Urusi

Mwanzoni filamu inayoitwa “The Death of Stalin” (kifo cha Stalin) ilikuwa imepangwa kuonyeshwa nchini Russia Januari 25, ambapo baadhi ya wakosoaji wa filamu hiyo wameiita ni kejeli ya kisiasa.

Wanasema ni kejeli ya kisiasa ya ‘kinyama’ katika kutafuta madaraka kufuatia kifo cha dicteta wa iliyokuwa Soviet mwaka 1953.

Hata hivyo filamu hiyo imepigwa marufuku na Wizara ya Utamaduni ya Serikali ya Kremlin.

mkurugenzi wa Uingereza Armando Lannucci ameeleza haya wakati wa tamasha la filamu la Sundance ambapo filamu hii ilifanyiwa tathmini.

Kadhalika wanafilamu wameiambia idhaa ya Russia VOA kwamba bado wanamatumaini kuwa filamu hizo zinaweza kuonyeshwa nchini na kuwa filamu hiyo inasimulia historia ya nchi hiyo.

Msimulizi wa sakata ya filamu hii anasema kuwa huko nchini Marekani, filamu hii “The Death of Stalin” itaonyeshwa baada ya wiki sita zijazo.

Ameongeza kuwa lakini nchini Russia bodi ya umma ya Wizara ya utamaduni kunauwezekano kuwa itazuia isionyeshwe nchini humo.

Yuri Polyakov, Mkuu wa Bodi ya Umma ya Wizara ya Utamaduni anasema: “Hii ni wazi kuwa wanalazimisha na kutukana hisia zetu za kiraia na kitaifa. … Kila mtu anasema hili, kufuatana na maoni ya kitasnia, hii ni filamu mbaya sana na uwongo mtupu. Hii ni nadharia ya ushindani wa kiitikadi na nchi yetu.”


XS
SM
MD
LG