Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:20

Felicien Kabuga, mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya Rwanda, akamatwa


Felicien Kabuga. Picha na AFP.
Felicien Kabuga. Picha na AFP.

Mshukiwa wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda, Felicien Kabuga, ambaye anashutumiwa kuwa mmoja wafadhili wakuu katika mauaji ya kiasi cha watu laki nane, alikamatwa Jumamosi karibu na mji mkuu wa Ufansa, Paris, baada ya kujificha kwa miaka 26, ilisema wizara ya sheria ya Ufaransa.

Kabuga, mwenye umri wa miaka 84, alikuwa akitafutwa sana nchini Rwanda na Marekani ilitoa tuzo ya dola milioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake.

Mshukiwa huyo alikuwa akiishi kwa kutumia kitambulisho bandia kwenye viunga vya Paris, kulingana na wizara ya sheria ya Ufaransa.

Maafisa polisi wa Ufaransa walimkamata Kabuga Jumamosi alfajiri kwa saa za Ufaransa, wizara ilisema.

Kabuga alifunguliwa rasmi mashtaka saba ya uhalifu mwaka 1997 ikiwemo mauaji ya halaiki, kitendo cha kushiriki mauaji ya halaiki na kuhamasisha wanamgambo kufanya mauaji ya halaiki.

Yote hayo yanahusiana na mauaji ya halaiki Rwanda mwaka 1994, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa katika mahakama inayofuatilia uhalifu Rwanda-IRMCT.

Mfanyabiashara huyo wa kabila wa Kihutu anashutumiwa kutoa fedha kwa wanamgambo ambao waliwauwa watu wa kabila la Watutsi na pia Wahutu wenye msimamo wa wastani wapatao laki nane katika siku 100 za mauaji mwaka 1994 nchini Rwanda.

Serikali ya Ufaransa imesema amekuwa mafichoni kwa muda mrefu na kwamba, kwa wakati mmoja, aliishi nchini Kenya kisiri.

-Imetayarishwa na Mkamiti Kibayasi, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG