Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:17

Felicien Kabuga afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali


Gari lililombeba Felicien Kabuga likielekea mahakamani mjini Paris, Ufaransa.
Gari lililombeba Felicien Kabuga likielekea mahakamani mjini Paris, Ufaransa.

Mshukiwa mkuu wa mauwaji ya halaiki ya Rwanda Felicien Kabuga Jumanne alifikishwa Mahakani mjini Paris chini ya ulinzi mkali.

Hayo yalijiri siku tatu tu baada ya kukamatwa na polisi wa Ufaransa akiwa kwenye nyumba yake katika kitongoji cha Asnieres sur Sien mjini humo alikokuwa akiishi na kujitambulisha kama mtu tofauti.

Vyanzo vya habari mjini Paris viliarifu kwamba jaji wa wa mahakama hiyo alianza kwa kueleza mchakato utakaofuatwa, katika kusikilizwa kwa hoja kuhusu iwapo Kabuga atahamishwa na kupelekwa kwa mfumo wa mahakama ya kimatiafa ya jinai, ICC au la.

Umoja wa Mataifa umepongeza maafisa waliomkamata Kabuga mwenye umri wa miaka 84 na ambaye amekuwa akisakwa kwa zaidi ya miongo miwili.

Felicien Kabuga
Felicien Kabuga

Kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa mataifa Michelle Bachelet amesema kuwa anatumai kukamatwa kwa Kabuga kutatoa motisha kwa mataifa mengine kuendelea kusaka washukiwa wa mauaji ya halaiki kote ulimwenguni.

Wataalam wa sheria wanasema kuwa mfumo wa sheria wa Ufaransa huenda ukachukua wiki kadhaa kabla ya Kabuga kufikishwa mbele ya mahakama maalum ya kimataifa iliyobuniwa na Umoja wa mataifa kusikiliza kesi za mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka wa 1994.

XS
SM
MD
LG