Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, amesema wawakilishi wakuu wa makundi 14 ya Palestina walifanya mazungumzo ya maridhiano mjini Beijing kuanzia Julai 21 hadi 23, na kutia saini tamko la Beijing juu ya kumaliza mgawanyiko na kuimarisha umoja wa kitaifa wa Palestina.
Mjini Washington, maafisa wa Marekani wanasema bado hawajapitia makubaliano hayo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, Jumanne alikiri kwamba Marekani imeitangaza Hamas kuwa taasisi ya kigaidi na Washington haioni nafasi yoyote kwa Hamas katika utawala wa baada ya vita wa Gaza.
Forum